Ushindani mkali watarajiwa katika uchaguzi wa Angola
19 Agosti 2022Matangazo
Chama hicho tawala nchini Angola MPLA kimekuwa madarakani kwa karibu miongo mitano.
Chama hicho kinachoongozwa na Joao Lourenco tangu mwaka 2017, kimeiongoza nchi hiyo ambayo ni muuzuaji wa pili mkubwa wa mafuta barani Afrika, tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1975 kutoka kwa Ureno.
Ila chama cha upinzani UNITA kwa sasa kina nguvu zaidi huku wananchi wakighadhabishwa na kushindwa kwa serikali kutumia utajiri wa mafuta wa nchi hiyo ili kuyafanya maisha kuwa bora.
Uchaguzi huo wa Angola utafanyika tarehe 24 Agosti ambapo rais na wabunge wapya watachaguliwa. Huu utakuwa uchaguzi wa tano chini ya mfumo wa vyama vingi vya kisiasa nchini humo tangu mwaka 1992.