Utajiri wa Lugha ni Lahaja
2 Juni 2015Matangazo
Miongoni mwa utajiri wa lugha ni lahaja zake zinazozungumzwa na watumiaji asili wa lugha hiyo kama kilivyo Kiswahili, lugha ya upwa wa Afrika Mashariki ambayo imesambaa kote Afrika Mashariki na hata ndani ya bara hilo.
Mohammed Khelef aliyehudhuria Kongamano la siku tatu la Kiswahili lililomalizika siku ya Jumanne (02.06.2015) mjini Bayreuth, kusini mwa Ujerumani, amekutana na mmoja wa wazungumzaji wa lahaja ya Kibajuni kutokea pwani ya Kenya, Hassan Edward. Na katika mazungumzo haya, Hassan anazungumzia tafauti zilizopo kati ya Kibajuni na lahaja nyengine za Kiswahili kwenye eneo hilo.
Kusikiliza mahojiano bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi:Mohammed Khelef
Mhariri:Josephat Charo