SiasaAsia
Viongozi wa China waahidi msaada zaidi kuchochea uchumi
30 Julai 2024Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika la habari la taifa kufuatia mkutano uliojikita katika kuimarisha ukuaji uchumi. China iko mbioni kufikia lengo lake la ukuaji uchumi kwa aslimia tano mwaka huu, kiwango kinachoelezwa na wataalamu kuwa kikubwa mno, huku taifa hilo lenye uchumi wa pili kwa ukubwa ulimwenguni likikabiliwa na changamoto zikiwemo soko la mali zisizohamishika lenye madeni, matumizi yaliyoongezeka na ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana. Mkutano wa leo wa maafisa wa vyeo vya juu wa chama cha Kikomunisti ni fursa kwa uongozi wa juu wa chama kutathmini hali ya sasa ya uchumi na kuweka mueleke mpya wa sera kwa nusu ya pili ya mwaka.