Viongozi wa G20 wanakutana Brazil kujadili mazingira
19 Novemba 2024Matangazo
Brazil ambayo ni mwenyeji wa mkutano huo iliandaa ajenda iliyoorodhesha masuala ya kipaumbele ambayo ni pamoja na kukabiliana na njaa na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na juhudi za kuyafanyia mageuzi mashirika ya Kimataifa. Hii leo Jumanne viongozi wanaokutana watajadili suala la maendeleo endelevu pamoja na mpango wa kuingia kwenye matumizi ya nishati safi na kuondokana na nishati zinazochafua mazingira. Viongozi hao wanalenga kuongeza hatua ya kupatikana makubaliano ya ufanisi ya kushughulikia ongezeko la joto duniani katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa unaoendelea Azerbaijan.