Viongozi wa nchi za karabu watoa ujumbe mkali kwa Israel
12 Novemba 2024Matangazo
Wito huo umetolewa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu, uliofanyika mjini Riyadh Saudi Arabia, na kutoa fursa kwa viongozi wake kuzungumza kwa sauti moja juu ya machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati.
Mwanamfalme wa Saudia bin Salman aitisha usitishwaji wa mapigano Gaza, Lebanon
Katika tamko lao la pamoja la kufunga mkutano wa kilele, viongozi wa mataifa hayo walisema amani ya kina katika eneo la Mashariki ya Kati, haiwezi kupatikana bila ya kukomeshwa ukaliaji wa kimabavu wa Israel katika maeneo yote ya ardhi ya Wapalestina, kuambatana na mipaka ya 1967, ikiwemo Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki, Ukanda wa Gaza na Milima ya Golan.