Wabunge Bunge la Ulaya wataka raia wa Urusi wasaidiwe
25 Julai 2023Katika barua yao kwa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Rais wa Baraza la Ulaya, Charles Michel, na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja huo, Josep Borell, wabunge hao kutoka vyama vya Social Democrat (SPD), chama cha siasa kali cha mrengo wa kushoto, na kile cha Kijani kinachotetea ulinzi wa mazingira, wamesema kuwa wanaamini ni jukumu la Umoja huo na mataifa mengine wanachama kulinda wanaopinga vita vya Urusi na kuwapa hifadhi.
Soma pia:Urusi yaituhumu Ukraine kufanya mashambulizi ya droni Moscow
Wabunge hao wametoa wito wa mashauriano kuhusu sera ya visa ya pamoja ili kurekebisha miongozo na taratibu za hifadhi ipasavyo.
Wabunge hao wamesema kamandi ya kijeshi ya Urusi inaripotiwa kujenga takriban vituo 13 vya vizuizi katika maeneo ya Ukraine ya Luhansk and Donetsk ambapo zaidi ya Warusi 600 waliokataakushiriki katika vita wanazuiliwa.