Wafanyakazi wa JKIA waliogama wakubali kurejea kazini Kenya
12 Septemba 2024Wafanyakazi wa uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya wamesitisha mgomo wao uliowakwamisha maelfu ya abiria, baada ya safari kadhaa za ndege kufutwa au kucheleweshwa.
Waziri wa usafiri wa Kenya Davis Chirchiri, amewaambia waandishi wa habari kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufikia makubaliano na menejiment kuhusu utaratibu wa kurudi kazini.
Somam pia: Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya wagoma
Wanachama wa chama cha wafanyakazi wa ndege waligoma kuhusiana na mpango wa kukabidhi uendeshaji wa operesheni za uwanja huo kwa kampuni ya Adani ya India kwa kipindi cha maiaka 30, kwa kampuni hiyo kuwekeza dola bilioni 1.85.
Kiongozi wa shirikisho la vyama vya wafanakazi la Kenya, Francis Atwoli, amesema wamepatiwa nyaraka kuhusu uwekezaji huo, ambao wataupitia kabla ya kuamua hatua inayokuja. Mgomo huo ulioanza usiku wa manane uliathiri vibaya safari za ndege.