Wagonjwa 171 wa mpox wakutwa na mpox Burundi
22 Agosti 2024Tangazo hilo linafuatia kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa nchini humo mwezi uliopita.
Waziri wa afya Polycarpe Ndayikeza ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, hadi sasa hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo.
Mwishoni mwa mwezi Julai, wagonjwa watatu walikutwa na mpox nchini Burundi huku wizara ya afya ikithibitisha wagonjwa wengine 153 waliokutwa na virusi vya homa ya mnamo mnamo Agosti 18.
Soma pia: Burundi yarekodi visa vya kwanza vya mpox
Wizara hiyo imetahadharisha kuwa ugonjwa wa mpox unaendelea kuenea kwa kasi na kwamba imeanzisha mchakato wa kuweka wodi maalum katika hospitali za wilaya ili kushughulikia wagonjwa wa homa ya nyani.
Soma pia: Tanzania yaimarisha hatua za kuzuia maambukizi ya Mpox
Afisa mmoja wa afya ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wagonjwa waliokutwa na homa ya nyani wanashukiwa kuwa na aina mpya ya kirusi cha mpox kinachosambaa kwa kasi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.