Wake za marais wa Afrika: Nguvu nyuma ya nguvu
Ingawa hawakuchaguliwa, bado wanao ushawishi mkubwa katika maamuzi. Baadhi ya wake za marais hata wanasemekana kuwa na ndoto za kuwa marais wenyewe. Wafuatao ni baadhi yao.
Grace Mugabe: Mwanzoni alibezwa, sasa anaogopwa
Kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo kichichini. Alizaa watoto wawili na Rais Mugabe akiwa bado katika ndoa na mke wake wa kwanza. Grace aliowana na Mugabe baada ya mke wake wa kwanza kufariki. Kwa sasa ni mwenyekiti wa tawi la wanawake la chama tawala ZANU-PF akiwa na ushawishi mkubwa. Wengi wanadhani atarithi madaraka ya mume wake, ingawa yeye anakanusha kuwa na azma hiyo.
Aisha Buhari: ''Mke wa Rais''
Wanaigeria wengi walifurahi walipomsikia Aisha Buhari akiahidi kuheshimu katiba, na kutojihusisha katika siasa. Kwamba badala yake atashughulikia tu masuala ya kijamii. Baada ya kuapishwa, Rais Buhari alivunjilia mbali ofisi ya Mke wa Rais akiita ufujaji wa fedha na isiyoendana na katiba.
Margaret Kenyatta: Kipenzi cha Umma
Wakenya wanampenda mke wa rais wao. Margaret Gakuo Kenyatta si mtu wa kujiweka mbele, bali ameelekeza juhudi katika kampeni ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Ni binti wa baba mkenya na mama mjerumani, ni mnyenyekevu na mwenye subira. Amekuwa mke wa ndoa wa Rais Kenyatta tangu mwaka 1991.
Ana Paula dos Santos: Kutoka mhudumu wa ndege hadi mtu mwenye madaraka
Ana Paula dos Santos alikuwa mhudumu wa ndege na mwanamitindo. alikutana na mme wake, Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos ndani ya ndege ya rais. Wapo wanaomsifu kama mtu anayejali ustawi wa wanawake na watoto, na wapo wanaokosoa mtindo wake wa maisha ya anasa. Yeye ni mke wa nne wa Rais Dos Santos, na wamezaa pamoja watoto watatu.
Dominique Ouattara: Mwanamke hatari?
Dominique Ouattara muda wote amependa kujichanganya na wenye nguvu. Alipokutana na Rais wa Ivory Coast Allasane Ouattara mnamo miaka ya 1980, Dominique alikuwa wakala wa kampuni ya kimataifa ya majumba. Alipoolewa na Ouattara, mwanamke huyo mfanyabiashara aliongeza nguvu katika uwanja wa siasa za Ivory Coast. Anatumia muda wake mwingi katika wakfu wake wa haki za watoto.
Janet Museveni: Mke wa Rais wa Maisha
Akiwa mke wa Rais wa miaka 30, Janet Museveni huenda ndiye mwanamke wa kiafrika alieishi Ikulu kwa muda mrefu zaidi. Baada ya mmewe, Yoweri Museveni kushinda uchaguzi mwingine wenye utata, Janet bado anao muda Ikulu. Akiwa mama wa watoto wanne, aliingia katika siasa hivi karibuni. Amekuwa mbunge tangu mwaka 2006, na mwezi Juni mmewe amemteuwa kuwa Waziri wa Elimu.
Marieme Faye Sall: Mama wa nyumbani
Mke wa Rais wa Senegal, Marieme Faye Sall (kulia) akiwa na mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama (kushoto), ndiye mke wa rais, wa kwanza mzawa wa Senegal. Watangulizi wake wote walikuwa na asili ya Ufaransa. Anatajwa kujikita zaidi katika kazi za nyumbani, bila kuingilia kazi za kisiasa za mmewe, Macky Sall. Hata hivyo, yeye na mmewe hukosolewa kwa maisha yao yanayozingatia ukale.
Marie Olive Lembe: Mpole na mwenye huruma
Kwa miaka mingi alikuwa mpenzi wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hadi mwaka 2006 walipofunga ndoa. Marie Olive Lembe di Sita ana watoto wawili na Rais Kabila. Anaaminika kuwa na uhusiano wa karibu na Jaynet Kabila, pacha wa mmewe Joseph, na ambaye anaaminika kuwa na ushawishi mkubwa kwa kaka yake. Kwa namna hiyo, DRC inao wanawake wawili walio na ushawishi kwa rais.
Afrika Kusini: Nani mke 'halisi' wa Rais Jacob Zuma?
Mwaka 2008, Rais Zuma alikimbia ''mchaka mchaka'' wa kuoa. Katika muda wa miaka minne aliowa wanawake watatu: Nompumelelo Zuma, Thobeka Zuma na Bongi Ngema-Zuma. Hao walikuja wakimkuta Sizakelle, mke wa Zuma wa muda mrefu. Hata mke wake wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, bado anatambulika kwa jina lake. Wakosoaji wanasema familia kubwa ya Zuma inawagharimu walipa kodi kiasi kikubwa cha fedha.